Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » BAADA ya Kupewa Talaka Jack Pentezel Afunguka na Kusema Haya Kuhusu Ndoa Hiyo iliyobuma

BAADA ya Kupewa Talaka Jack Pentezel Afunguka na Kusema Haya Kuhusu Ndoa Hiyo iliyobuma

BAADA ya kupewa talaka na aliyekuwa mumewe, Gadna Dibibi, mwigizaji Jacqueline Pentezel ‘Jack Chuz’ ameamua kufunguka na kuweka wazi kuwa hayuko tayari kuolewa tena.

Jack alisema, kwa muda aliodumu kwenye ndoa ameshaona raha na karaha yake hivyo suala la kuolewa tena sasa hivi halipo akilini mwake.

“Katika ndoa lazima kuwe na mabaya na mazuri, hata hivyo siwezi kusema ndoa ni chungu hapana, ila mimi kwa sasa hivi nimeona nipumzike kwanza sitaki tena ndoa labda kwa hapo baadaye nitakapojipanga tena upya,” alisema Jack.

Jack alidumu na mumewe huyo kwa miaka miwili na nusu kabla ya kupewa talaka hivi karibuni huku chanzo kikiwa ni kusalitiana katika mapenzi. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips