Imekuwa sio siri tena Kwa Lulu kuvutiwa kimapenzi na mwimbaji ,wenye
asili ya canada anayefanya kazi zake za ki muziki huko nchini marekani,
suala la lulu kumzimia jamaa huyu ni miaka zaidi ya mitano sasa na ndilo
jambo ambalo team ya Saa mbovu inaona sio la mzaha mzaha hata kidogo
mana miaka 5 sasa kauli za lulu zipo pale pale akilia na penzi la
beiber!!.
Kipindi cha nyuma mnamo mwezi wa nane tarehe 17 mwaka 2011 mtandao wa blog ya zamaradi mketema uliweka habari hii hapa chini.
Mwaka jana tu tena mtandao wa timesfm.com unaomilikiwa na radio times nao ukadondosha udambwi dambwi huo!!
Siku nyingine tena mtandao wa bongo5 unaojihusisha na habari za burudani hapa nchini ukafunguka bila hiyana kuhusu saga hili.
Hii imefanya Saa Mbovu kufanya kiutafiti kidogo imegundua Lulu kaoza ,
akajifia na kujizika kabisa kwa kijana huyu mkali wa R&B mana
imefikia hatua kaweka nadhiri kabisa kila jumatatu kupitia mtandao wake
wa instagram ni spesho post kwa ajili ya justine beiber na jumatatu
iliyopita hichi ndicho alicho post.
Huku akiandika "Uliamua kuni follow kwa Hiari Yako....vumilia Na Post
Zangu Tafadhali" hii inatoka na wadau ambao ni follower wa kurasa yake
kuwa wakichana mbaya kila akitupia vitu vya huyu jamaa kiasi cha
kupelekea kuwa ambia watakoma naye na kula sana maliamo kama wanaona
kichefu chefu na moyo wake ulipo dondokea!! hahahaha kweli hapa SAA
MBOVU ISHAPOTEZA MAJIRA.
0 comments:
Post a Comment