“Kuna watu ambao wanadai na kuandika hata katika mitandao ya kijamii kuwa eti ofisi za Kanumba The Great Films zimefungwa na hazipo tena, si kweli kodi ni kubwa sana hivyo tumehamishia Kimara Temboni,”anasema Mama Kanumba.
Mama Kanumba amesema kuwa ofisi hiyo inafanya kazi wala haijafungwa na kwa uhakika ni kwamba kuna filamu ambayo imekamilika na itatoka hivi karibuni chini ya kampuni, filamu hiyo imewashirikisha wasanii Flora Mtegoa, Mohamed Mwikongi ‘Frank’, Rose Ndauka na wasanii wengine. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment