Manchester United
 ni kama haina bahati msimu huu, mpaka sasa bado haipo katika kiwango 
kizuri cha uchezaji na inakamata nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi 
kuu ya England.
Pamoja na kutokuwa na kiwango kizuri lakini bosi wa klabu hiyo Louis Van Gaal ameweza kuibuka mshindi katika tuzo maarufu ya Anton Geesink ambayo hutolewa nchini Uholanzi.
Tuzo hiyo maalum hutolewa kwa mtu, mji au kundi la watu lililofanya vema katika michezo mbalimbali.
Van Gaal ambaye kikosi chake cha Man United
 hakiko katika kiwango kizuri msimu huu amepewa tuzo hiyo baada ya 
Uholanzi kuonyesha kiwango bora na kushika nafasi ya tatu katika Kombe 
la Dunia nchini Brazil, mwaka jana.
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment