nia-royalty
Vyanzo vilivyo karibu na mastaa hao vimeiambia TMZ kuwa Chris na Karrueche wamekuwa wakizungumza kuhusu mtoto kwa miaka miwili sasa na mrembo huyo alikuwa tayari kumzalia kama angetimiza matakwa yake.
Vyanzo hivyo vimeuambia mtandao huo kuwa KT ni msichana anayeamini katika ndoa kabla ya kupata mtoto.
Karrueche pia alikuwa na wasiwasi wa kuharibu career yake ya filamu.
Pamoja na kwamba hakuwa tayari, Karrueche aliendelea kuamini kuwa yeye na Chris wangepata watoto pamoja siku za usoni. Chanzo kimoja kimedai kuwa habari hiyo imemvunja moyo kwa kiasi kikubwa.
Wakati huo huo jina la mtoto wa Chris Brown kwa mujibu wa mtandao huo ni Royalty. Mama wa mtoto huyo mwenye miezi 9 anaitwa Nia Amey mwenye miaka 31.
Nia anadaiwa kuwa huongea na Chris mara kwa mara na anamtaka mzazi mwenzie kumlea mtoto wao bila kujificha. Mama na mtoto huyo wanaishi Texas, na Chris anasema atafurahi kuwafuata kuungana nao.
Karrueche hakuwa na wazo lolote kuhusu mtoto huyo na ndio maana aliamua kuachana naye kwa mara nyingine tena.
“Listen. One can only take so much. The best of luck to Chris and his family. No baby drama for me,” alitweet. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment