Akifafanua kauli yake kwa mapana , Barnaba alieleza kwamba Diamond hajui kuimba kufuatana na alama zote muhimu za muziki, bali hutumia mtindo flani wa kuimba 'kiujanja', mtindo ambao kwa wanaojua kuimba muziki technically huwa wanautumia pale wanapofeli kufuata kanuni za uimbaji wakati wakiimba.
Hata hivyo, alimsifia kwa kuwa 'mjanja' na kuweza kufanya muziki wake kuvutia na kuleta ladha.
Orodha ya wasanii ambao aliwatolea maoni na kusema ni wasanii anaowakubali sana ni pamoja na, Diamond, Ally Kiba, Ditto, Amini na yeye mwenyewe. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment