Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Askari Polisi wa Kike Avuliwa Nguo na Kuachwa Mtupu, Watu Wanane Wafikishwa Kortini

Askari Polisi wa Kike Avuliwa Nguo na Kuachwa Mtupu, Watu Wanane Wafikishwa Kortini

Wafanyabiashara watatu na wanachuo watano wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Singida wakikabiliwa na mashitaka ya kumdhalilisha kupindukia askari polisi wa kike na kumsababishia maumivu makali mwilini.

Mwanasheria wa Serikali, Petrida Mutta alidai mbele ya Hakimu Joyce Minde, kwamba kwa pamoja, washitakiwa hao walimfanyia unyama askari huyo kwa kumvua nguo zote na kumwacha mtupu kisha kumshambulia na kumsababishia maumivu makali mwilini.

Waliopandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi, Joyce Minde, ni Jasmin Iddi (40), Abdallah Hamduni (26), Ramadhani Bakari (32) wote wafanyabiashara wa mjini hapa pamoja na dereva, Saidi Saidi (50) .
Wengine ni Aurelia Adolf Mushi (20), Grace Daniel Paul (21), Happiness Kiluvya (23), Jackline John (20) na Constansia Masaki (21) wanaodaiwa ni wanachuo katika moja ya vyuo vya elimu ya juu mjini Singida.

Mwanasheria wa serikali, alidai wakati wote wa kitendo hicho cha udhalilishaji, polisi huyo, alikuwa akichukuliwa picha za video huku akiwa mtupu na kuzisambaza kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

Tukio hilo inadaiwa lilifanyika Februari 14, mwaka huu saa 11.30 jioni ambako kwa mujibu wa Mwendesha Mashitaka, inadaiwa polisi huyo wa kike alikutwa akiwa na mume wa mshitakiwa, Jasmin wakiwa kando ya Ziwa Singidani wakivinjari siku hiyo ya Wapendanao.
Hata hivyo, mume ambaye jina halikupatikana, inadaiwa alitoroka. Mutta alidai mbele ya mahakama hiyo kuwa kitendo walichofanya washitakiwa ni kinyume na Kanuni ya Adhabu 138 A kifungu cha 16 cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai kama kilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002. Wote walikana mashitaka WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips