Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Mungu ni Mkubwa: Mama yake Diamond Arejeshwa toka India......Afya yake kwa sasa inatia Moyo

Mungu ni Mkubwa: Mama yake Diamond Arejeshwa toka India......Afya yake kwa sasa inatia Moyo

Mungu ni  mkubwa :Mama mzazi wa Supastaa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim ‘Sandra’, amerejeshwa Bongo kutoka India ambapo afya yake imetengemaa.
Habari kutoka chanzo cha kuaminika ndani ya familia ya jamaa huyo, kimesema kwamba tayari
 Sandra amesharejea katika hali yake ya kawaida na ndiyo maana akarudi Bongo baada ya kulazwa hospitalini nchini India kwa kusumbuliwa na ugonjwa wa kupooza.

Mwanafamilia huyo alisema kwamba, Diamond na mama yake walirejea nchini wikiendi iliyopita baada ya kufanyiwa matibabu ya kina na madaktari kujiridhisha kwa hali ya juu dhidi ya afya yake ambapo waligundua hali aliyonayo kwa sasa imetengemaa hivyo wakamruhusu kurejea kuungana na familia yake.

Habari zilieleza kuwa kwa sasa bimkubwa huyo yupo fiti na anaendelea na mazoezi ya kawaida huku akimalizia dawa alizopewa na wataalam hao wa afya. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips