Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » JWTZ yaapa Kupambana na Majambazi Wanao pora Silaha za Askari

JWTZ yaapa Kupambana na Majambazi Wanao pora Silaha za Askari

Jeshi la wananchi nchini (JWTZ) kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama nchini limeahidi kukabiliana na makundi ya watu wanaodaiwa kuwa majambazi sugu ambao wanapora silaha za ....



askari huku wengine wakiuawa hatua ambayo imeanza kutishia usalama wa nchi.

Akizungumza jijini Tanga kufuatia hivi karibuni makundi hayo kupora silaha na kisha kuua askari huko Rufiji mkoani Pwani na wengine wakipora askari wawili silaha nyakati za usiku jijini Tanga na kisha kuwadhuru hatua ambayo imesababisha kulazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tanga bombo,katibu mkuu wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa  JOB MASIMA amesema vyombo vya ulinzi vitakaa na kuhakikisha kuwa mtandao huu unapatikana ili kurejesha silaha hizo.

Hata hivyo katibu mkuu amekana vikali kuwa huenda makundi haya ya uhalifu yanayojihusisha na kupora silaha askari ni wahitimu waliopitia mafunzo ya jeshi la kujenga taifa JKT ambao baadhi yao hawakupata ajira baada ya kurudu uraiani na kuongeza kuwa hata wanaojihusisha na ugaidi sio wote ambao wamepitia mafunzo ya kijeshi.WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips