Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Aunt Ezekiel Aporomosha Matusi Mazito

Aunt Ezekiel Aporomosha Matusi Mazito

Mrembo na mwigizaji wa filamu za kibongo, Aunt ezekiel amejikuta akitoa maneno makali baada ya mashabiki wake kumshabulia kwa maneno baada ya kuweka mtandaoni picha ikimuonyesha amevalia kinguo ambacho kwa maoni ya mashabiki hao hakistahili kuvaliwa na mwanamke mjamzito na kibaya zaidi alionekana mkononi ameshika chupa ambapo wengi waliiona kama niyakilevi.

Aunty Ezekiel alibandika picha hiyo hapo juu akiwa na jamaa kwenye ukurasa wake mtandaoni na kuandika maneno “My best friend,my love,my kimoko I love him so much”

Baada ya kubandika ujumbe huo baadhi ya mashabiki wake walionyeshwa kukerwa na mavazi na sehemu alikokuwepo nakumtaka atulie nyumbani alee mimba yake kwani kwasasa inaonekana kuwa na ya zaidi ya miezi nane na wiki kadhaa.

“Ungetulia  tu nyumbani ukasubiri kujifungua salama,mjamzito kuzurura namna hiyo na mijanaume sio poa kabisa tena na kilaji mkononi harafu pia hata hayo mavazi mmmh!!” alisema mmoja wa shabiki na kuungwa mkono na wengine wengi.

Baada ya muda kidogo aunty ezekel akaibuka na  kuandika ; “Plz msiwe bac mnaongea kitu kabla ujajua undani wake, ni vizuri kuuliza kuliko kuandika tu ilimradi na wewe uonekane umeongea hiyo nguo ni special kwa mama mjamzito na hapo juu inampira wakutosha tu na mapajani ndio inabana sasa”

Lakini majibu hayo yalionekana kuamsha maneno zaidi ya kumponda Aunty ambae nae mwishoni  alionekana kushindwa kuvumilia na kutoa matusi  mazito ambayo sio busara kuyabandika hapa. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips