Hatimaye Nay wa Mitego amezungumzia scandal iliyokuwa ikimhusu mchumba
wake aitwaye Siwema ambaye mwezi uliopita ilisambaa video na picha
kwenye mtandao wa Instagram inayomuonesha akivishwa pete na pedeshee.
Maelezo kuhusu video/picha hizi yalisema:
“Siwema demu wa Nay Wa Mitego amevalishwa pete ya uchumba na jibaba (
pedeshee ) linalomuweka mjini na ndilo lililomnunulia magari mwanzo
aina ya Verosa na baadaye Kluger halafu Verosa akampa Nay wa Mitego,
sasa hivi kamnunulia Lexus harrier… Inasemekana Nay pia analelewa na
huyo dingi maana amekubalije amegewe demu na kuhongwa gari alilohongwa
demu wake.”
Pia kupitia mtandao huo, picha za msichana huyo zinazomuonesha akiwa nusu utupu zilisambaa.
Akiongea kwenye kipindi cha So So Fresh cha Clouds FM Ijumaa hii, Nay alisema ni kweli Siwema alimkosea lakini amemsamehe.
“Mimi Siwema ni mwanamke ambaye nampenda kila mtu anafahamu maybe
ndio maana ilikuja kuwa tatizo. Kuna vitu vilitokea mimi nilikuwa
sifahamu kama nilivyosema kuna watu wakanifuata wenye nia zao sielewi
mtu alikuwa na nia gani wakiviweka Instagram na kwenye mtandao. Mimi
mwanamke wangu najua alinikosea. Sikujua kilichokuwa kinaendelea lakini
hakuweka wazi. Ni kitu ambacho kilitokea kabla ya mimi kuwa naye lakini
hakuwahi kuniambia kwamba kilitokea mpaka wakafikia hatua ya design
hiyo, hilo ni kosa ambalo alinikosea. Tuliyamaliza, mimi ni gangster
ambaye na nina mwanamke ambaye nampenda. Huwezi kumwacha mwanamke
kwasababu ya kitu ambacho ni cha historia, sidhani kama ni fair. Pia ni
mwanamke ambaye mimi nipo naye kwasababu tunapendana halafu ni mwanamke
ambaye ananielewa na tunaelewana na ndio maana niliamua kumweka wazi
kila mtu anamfahamu. Hata kama itakuwa vyovyote vile, siwezi kumwacha
hata siku moja. Kweli ni kosa kubwa ambalo linahitaji moyo kwaajili ya
kumsamehe mtu lakini naamini nimefunzwa kusamehe kwenye mahusiano, hili
ni la kwanza acha lipite mwenyezi Mungu atusaidie tuendelee kudumu. Mimi
nipo bado na Wema na maisha yanaendelea.”
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment