Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Showing posts with label Ray. Show all posts
Showing posts with label Ray. Show all posts

Ray Awapa Makavu UKAWA

Vincent Kigosi ‘Ray’ 
Staa wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ ameendelea kushusha maneno kwa chama kinachounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) baada ya kufunguka hadharani kuwa hawakuwa na sera ambazo zingemfanya aendelee kubaki.

Staa huyo ambaye kwa sasa amerudi Chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema kurudi kwake CCM hakumaanishi kama amehongwa kama watu wanavyoendelea kusambaza habari hizo bali amekwenda kutokana na kuvutiwa na sera.

“Naomba nieleweke kuwa dhamira yangu ya kubaki Ukawa ndiyo ilikuwa ikinisuta. Nikiwa kama mmoja wa wasanii, nimevutiwa na sera za CCM hasa kwa upande wa wasanii ambapo Mgombea Urais, Magufuli (John Pombe) alisema moja ya sera zao ni kujali maslahi kwa wasanii na kuwafungulia mfuko maalum utakaowashughulikia,” alisema Ray. 3

Aunti Ezekiel na Vincent Kigosi Kutoka UKAWA Wajiunga na Kampeni za CCM

Zikiwa zimebaki takribani siku 39 kuelekea siku ya Kupiga kura. Wasanii wawili wa tasnia ya Maigizo waliokuwa katika Kampeni za Mh Edward Lowassa wa CHADEMA ghafla wameamia kwenye Kampeni za Mh John P. Magufuli wa CCM.

Hii imethibitishwa na mmoja wa wasanii hao, yaani Anti Ezekiel kupitia kwenye ukurasa wake wa Twitter.      (Auntezeofficial)

Ni stori ya kisiasa ambayo ilianza kuchukua headlines kwenye mitandao mbalimbali kuhusu wasanii wawili wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel na Vicent Kigosi aka Ray kuondoka UKAWA na kuhamia chama cha Mapinduzi.

Baada ya taarifa hizo kuchukua nafasi kubwa kwenye mitandao sasa ripota wa millardayo.com amezungumza na Steve Nyerere ambaye ni mwenyekiti wa kampeni ya Mama ongea na Mwanao…’Ndugu zetu wakina Vicent Kigosi na Aunt Ezekiel walitoroka wamerudi CCM kabla hawajatangaza lakini watatangaza wamerudi kwa kishindo kikubwa wanaamini bila hapo walipofika bila nguvu ya Mh Jakaya Mrisho Kikwete wasingiweza kufika‘ – Steve Nyerere

‘Kwa hiyo nataka kuwaambia watanzania kuwa hao watu wamerudi katika chama cha mapinduzi na wala msidanganywe pilika pilika za huku na kule hawa watu ni wanachama wa CCM hai walitoroka na sifa ya kutoroka ni kukosa nidhani kwa sisi wazazi ambao tuna watoto , mtoto akitoroka unatakiwa umpe adhabu ili siku nyingi afahamu njia ya sahihi na njia sahihi ni chama cha Mapinduzi ambacho kina Dkt John Pombe Magufuli na Mama Samia Suluhu’ – Steve Nyerere

Chanzo: JF by DemiGod 3

Licha ya Kupata Bwana Mpya; Johari: Siachani na Ray!

Ray na Johari Katika Pozi
SIKU chache baada ya kupenyezwa kwa madai ya kupata bwana mpya, staa wa filamu Bongo, Blandina William Chagula ‘Johari’ ameibuka na kuweka wazi kuwa kamwe hafikirii wala hana mpango wa kuachana na msanii mwenzake, Vincent Kigosi ‘Ray’ katika masuala ya kazi.

Akianika mwanya’ na Risasi Jumamosi hivi karibuni ndani ya ofisi zake, Sinza-Mori jijini Dar, Johari alisema hawezi kuruhusu mapenzi yatawale maisha yake na kusahau kazi.

“Siondoki RJ, kama kuna mtu anatarajia nitoke hapa eti kisa mambo ya mapenzi, anajidanganya kabisa, sifikirii kuachana na Ray kikazi, ni mtu muhimu sana, mapenzi hayawezi kutawala maisha yangu, yeye atabaki na mpenzi wake na mimi nitaendelea na mpenzi wangu,” alisema Johari.

Ray kwa sasa ameshaonesha upande na kukiri kukolea kwenye penzi la mwigizaji  Chuchu Hans na tayari ameshajipambanua kuwa wana mipango endelevu maishani mwao.

Chanzo: GPL
3

MWIGIZAJI Ray Afichua Siri ya MREMBO Chuchu Hans!

Muigizaji mahiri wa kiume hapa Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’amefichua siri iliyomfanya kunasa kwa staa mwenzake Chuchu Hans, na hata kupata msukumo wa kumuweka hadharani tofauti na tabia yake ya nyuma ya kutopenda kumuanika mpenzi wake.

Akizungumza na gazeti la Risasi akiwa kwenye tamasha la kimataifa la Filamu ‘ZIFF’ lililofanyika visiwani Zanzibar, Ray alisema kilichomsukuma kumuanika Chuchu ni mambo yake adimu ambayo huwezi kupata kwa mwanamke mwingine.

Alisema anamuona kuwa na tabia zote za mke, ndiyo maana aliweza kumtambulisha kwa jamii kwa kuwa ana imani naye kwa kila kitu hivyo yuko huru watu kumfahamu.

“Bwana huyu mwanamke ana vitu vyake adimu sana, na kwa kweli nampenda na ana chembechembe zote za kuwa mke ndiyo maana nilikuwa huru kumuweka wazi bila wasiwasi wowote,” alisema Ray ambaye pia aliwahi kutoka kimapenzi na Johari.

Chano:GPL 3
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips