Vincent Kigosi ‘Ray’ |
Staa huyo ambaye kwa sasa amerudi Chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema kurudi kwake CCM hakumaanishi kama amehongwa kama watu wanavyoendelea kusambaza habari hizo bali amekwenda kutokana na kuvutiwa na sera.
“Naomba nieleweke kuwa dhamira yangu ya kubaki Ukawa ndiyo ilikuwa ikinisuta. Nikiwa kama mmoja wa wasanii, nimevutiwa na sera za CCM hasa kwa upande wa wasanii ambapo Mgombea Urais, Magufuli (John Pombe) alisema moja ya sera zao ni kujali maslahi kwa wasanii na kuwafungulia mfuko maalum utakaowashughulikia,” alisema Ray. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment