Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum toka Singida, Christina Mughwai Lissu(CHADEMA) amefariki dunia kwa ugonjwa wa kansa.
Marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa cancer tangu mwaka jana.
Tundu Lissu Ameandika Hivi:
Waheshimiwa nawasalimu kutoka Kibondo.
Nina habari zisizokuwa njema. Dada yangu na aliyekuwa Mbunge wetu wa
Viti Maalu m Mh. Christina Lissu Mughwai amefariki dunia muda mfupi
uliopita katika hospitali ya Aga Khan Dar.
Marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa cancer tangu mwaka jana.
Kwa sasa niko nje ya Dar na ndio kwanza taarifa hizi zimenifikia, sina
taarifa zaidi juu ya mipango ya mazishi, etc. Tutawataarifu baada ya
familia kuwa tumeshauriana.
Tundu Lissu.
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment