Hili suala nimelifikiria kwa kipindi kirefu sana., naona mifano mingi
kupitia kwa marafiki zangu na hata ndugu zangu na watu wangu wa karibu.
Unakuta mwanaume upo kwenye mahusiano ya kawaida na msichana bado
hamjafunga ndoa alafu migogoro na kuachana mara kwa mara, tena unakuta
wewe ndo unaachwa na huyo mwanamke alafu unambembeleza mnarudiana.
Mwanamke haonyeshi upendo wowote kwako lakini wewe unaendelea kumpenda na kumjali sana. Hayo yote haujifunzi unaamua kumng'ang'ania na mwisho wa siku mnafunga ndoa.
Hivi mwanamke kama huyo akiwa anakusaliti katika ndoa utamlaumu nani.?
Kuna rafiki yangu wa karibu aliwahi kuoa mwanamke wa aina hiyo, ndoa yao
ilidumu kwa miaka 5 tu na mimi nilikuwa best man wake, maana mwisho wa
siku ikaja kugundulika hata watoto wawili ambao walikuwa wameshazaa
hawakuwa wa kwake.
Wanaume tujifunze jamani tunapochagua mwanamke wa kuishi naye kwa maisha
yote, tusiziendekeze akili za nyege wakati wa kuchagua wenzi wa maisha.
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment