Kiongozi wa mfara huo Willy Mwandwa na wenzake Kizito Bombo na Hanru Makau wamesema walilazimika kuingia kisiwani Pemba kwa kutumia bandari bubu na kujikuta wapo mikononi mwa vyombo vya ulinzi na usalama kutokana na kuharibikiwa na mashua yao waliokuwa wakisafiria kutoka Mombasa kwenda Unguja kufanya kazi katika kambuni yao ya ujenzi ilioko huko na kudai wao ni wasafiri halali hivyo wameshangaa kukamatwa.
Kwa upande wake Afisa wa Uhamiaji mkoa Kaskazini Pemba amesema wamewakamata vijana hao kucheki kama wana paspoti za kuingilia na endapo watajiridhisha kuwa wana vibali wata wachia kuendelea na safari yao na kuwataka watu wanao ingia au kutoka kisiwani pemba kuacha tabia ya kutumia bandari bubu. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment