Uchaguzi wa Meya
wa Jiji la Dar es salaam umezidi kuchukua vichwa vya habari baada ya
kuahirishwa mara kadhaa na hata mara ya mwisho kuibuka kwa vurugu ambazo
zilipelekea baadhi ya Wabunge wa Chadema na Madiwani wake kufikishwa mahakamani na baadae kuachiliwa kwa dhamana.
March 10 2016 Mbunge wa Jimbo la Ubungo (Chadema), Saed Kubenea amehitajika polisi kwa tuhuma za kuhusika na vurugu wakati uchaguzi huo ulipoahirishwa February 27 2016. Saed Kubenea ameelezea kuhusiana na wito huo wa polisi kwa ajili ya kujibu tuhuma hizo na amesimulia ilivyokuwa….
>>>’Nimefuatwa
na askari kama sita wakiniambia kwamba niko chini ya ulinzi
ninahitajika makao makuu ya polisi Dar es salam nikahoji kosa langu ni
nini? wakasema nikajibu tuhuma juu ya vurugu zilizotokea katika uchaguzi
wa Meya wa Dar es salaam‘:-Saed Kubenea
Pia ameeleza kwamba hapo awali wakati tukio linatokea yeye
hakuwa kwenye orodha ya washitakiwa kwa hiyo anakwenda kuwasikiliza na
kama atapelekwa mahakamani anaamini haki itatendeka, Kubenea ameeleza..
>>>’ninachokumbuka
mimi nilifika makao makuu polisi kuwasilisha malalamiko juu ya amri
iliyotolewa kwamba uchaguzi ule uzuiliwe, niliwathibitishia polisi
kwamba amri ile ilikuwa haramu na ilikuwa imeexipire kwa hiyo ni lazima
wachukue hatua za kisheria dhidi ya wahusika, na SP Ndalama ambaye ni
mkuu wa upelelezi wa mkoa wa kipolisi Ilala alikuwepo na alinipa orodha
ya watu wanaotakiwa mimi jina langu halikuwemo‘:-Saed Kubenea
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment