Mtu wangu wa nguvu bado millardayo.com
inaendelea kukuletea kila linaloendelea duniani, iwe usiku au mchana,
nimekutana na list nyingine ya TOP 5 ya madaraja hatari zaidi duniani ya watembea kwa miguu, hii ni list kutoka mtandao wa www.wonderslist.com.
5- Trift Bridge – Switzerland
Daraja hili lilijengwa mwaka 2004, na
kukarabatia au kufanyiwa matengeneza kwa awamu ya pili mwaka 20o9, hili
linatajwa kutokuwa daraja salama kwa binadamu kukatisha, kwani usalama
wake mdogo sana, hata kamba zilizopo pembeni sio salama sana kuziamini
kama zina msaada.
4- Musou Tsuribashi Bridge – Japan
Hili ni daraja ambalo lina miaka zaidi
ya 50 toka litengenezwe mwaka 1950, limetengenezwa kwa bodi na kamba
ambazo zinatajwa kuwa sio imara sana, hupitwa na watu mara kadhaa, ila
unashauriwa kama unataka kufanya hivyo ni lazima ufikirie mara tatu
kufikia maamuzi hayo.
3- Aiguille du Midi – Ufaransa
Daraja hili lipo Ufaransa
na kama una matatizo ya moyo hushauriwi kuwa na mipango ya kupita
daraja hilo, kwa sababu njia yake ni nyembamba na lina urefu wa
futi 12600 kutoka usawa wa bahari, daraja hili ni tishio kwa kila mmoja
kutokana na urefu wake.
2- Kakum National Park Canopy Walkway – Ghana
Daraja hili lipo katika hifadhi ya taifa nchini Ghana,
lina urefu wa futi 76 kutoka chini na limetengenezwa kwa mbao na kamba,
lakini daraja hili mara nyingi hupendwa kutumiwa na watalii. Hili ndio
daraja hatari kwa watembea kwa miguu lilikuwepo Afrika.
1- Marienbruecke – Ujerumani
Licha ya kuwa kuna materio ya chuma baadhi yametumika kutengeneza daraja hilo ambalo lipo katika milima ya Bavarian
na inaunganisha kati ya kilele cha mlima mmoja na mwingine, lakini sio
salama. Kama utakatisha daraja hilo lazima mapigo ya moyo yaongezekea.
0 comments:
Post a Comment