Kauli hiyo imetolewa leo jijini Mwanza na mwenyekiti wa Chadema taifa Mh. Freeman Mbowe akiwa pamoja na Waziri mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye pamoja na aliyekuwa mgombea urais kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) akiungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) Mh. Edward Lowassa.
Naye Mchungaji Charles Lugiko ambaye ni baba wa marehemu Alphone Mawazo amelaani kitendo cha askari polisi kwenda hadi nyumbani kwake eneo la Nyegezi na kuwatawanya waombolezaji waliokuwa wamekusanyika nyumbani kwa ajili ya kuuaga mwili wa marehemu Mawazo.
Alphonce Mawazo aliuawa kikatili kwa kukatwa mapanga na mashoka na watu wasiojulikana Novemba 14 mwaka huu katika kijiji cha katoro wilayani Geita. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment