Kahama. Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli amesema waliofanya
utafiti wamempunja asilimia kwani ana uhakika wa kushinda kwa asilimia
95 na si 65 kama zilivyotajwa kwa kuwa wananchi wanampenda, naye yuko
tayari kufanya kazi ili kuwaletea maendeleo.
Akizungumza jana mjini Kahama, Dk Magufuli alisema: “Wapo wanaosema
nimeshinda kwa asilimia 65, mimi ninasema nitashinda kwa asilimia 95,
ninachoomba mjitokeze kwa wingi siku ya kupiga kura ili nitangazwe
mshindi, ninawaahidi kwamba nitawatumikia na kujenga Tanzania mpya.”
Hivi karibuni, taasisi ya Twaweza ilitoa utafiti wake uliompa nafasi
ushindi wa asilimia 65 huku mpinzani wake, Edward Lowassa akipata
asilimia 25 na mgombea wa ACT –Wazalendo akipata asilimia 0.3.
Baadaye, taasisi ya Ipsos (Synovate) ilitoa utafiti wake ukionyesha
kwamba alishinda kwa asilimia 62 huku Lowassa akipata asilimia 31 na
Anna Mghwira akipata asilimia 0.3.
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment