Nimekutana na stori kutoka Marekani New York ambako wafungwa wawili waliohukumiwa kifungo cha maisha wametoroka jela siku chache zilizopita huku wakiwaacha maaskari magereza kwenye mshangao wakiwa hawaelewi ishu hiyo imetokeaje.
Stori kwenye headlines wakati huu jijini New York ni malalamiko kutokwa kwa wafungwa wa Clinton Correctional Facility amabao wanawalalamikia maaskari hao kwa kuwatesa na kuwafanyia vitendo vya kuhatarisha maisha yao kwa nia ya kutafuta ukweli kuhusu wafungwa hao waliotoroka.
Wafungwa waliobaki walikuwa wakichukuliwa mmoja mmoja na kupelekwa kwenye chumba maalum ambako walikuwa wakipigwa, wakikabwa koo, wakibamizwa kwenye ukuta na vitendo vingine vya mateso na maaskari hao na ikiwa wakishindwa kutoa taarifa ambayo maaskari hao wanaitaka basi vipigo na mateso vinaongezeka.
Baadhi ya wafungwa wakaamua kupeleka mashitaka yako mbele ya Ofisa Mkuu wa Magereza, taarifa ikawafikia Serekali na sasa hivi maaskari hao wako chini ya uchunguzi.
Hapa chini nimekusogezea kipande cha video kinachoelezea jinsi hali ilivyo huko New York.
0 comments:
Post a Comment