Kocha wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho amekwenda mbali zaidi baada ya kumpiga marufuku daktari wa timu Eva Carneiro kuwa sehemu ya kikosi cha Chelsea wakati wa mazoezi na kwenye mechi mbalimbali za kiushindani n ahata kwenye hoteli ambayo timu itakuwa ikifikia kabla ya mechi .
Hatua hii inakuja baada ya kocha huyo kumshutumu Eva kwa kitendo cha kukimbia uwanjani kumtibu Eden Hazard akidhani ameumia vibaya wakati mchezaji huyo hakuwa ameumia kiasi cha kulazimu kutibiwa na kutoka uwanjani .
Mourinho amechukua hatua hii baada ya kile alichokiita hali ya watu walioko nae kwenye bench la ufundi la klabu hiyo kutoujua vyema mchezo wa soka kiasi cha kuigharimu timu hiyo na kuinyima ushindi au kuifanya ipoteze mchezo .
Mourinho alimshutumu Eva kwa kuingia uwanjani kumtibu Hazard ambaye alikuwa hajaumia bali alikuwa amechoka na hivyo kumfanya atoke uwanjani na kusubiri ruhusa ya refa kurudi huku Chelsea ikiwa pungufu katika mazingira ambayo timu hiyo ingeweza kupoteza mchezo .
Hii si mara ya kwanza kwa Mourinho kulumbana na madaktari wa timu yake na wakati mwingine hata timu pinzani kwani kwa nyakati tofauti akiwa kocha wa Chelsea , Inter Milan na Real Madrid wamewahi kuingia kwenye malumbano na matabibu .WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment