Sasa kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo, Mh Zitto Kabwe leo amefunguka kuhusu chama chake kumteua mgombea au kuunga mkono mgombea cha chama kingine.
Kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter amewahabarisha wananchi kwa kusema…’Chama chetu kitateua mgombea au kuunga mkono mgombea wa chama kingine kwa maamuzi ya VIKAO vya chama. Kama Kiongozi wa chama sina mamlaka yeyote yale kutangaza mtu kuwa mgombea wetu’ – @zittokabwe
Hivi sasa Uongozi mzima wa Chama upo kwenye retreat ili kujipanga na uchaguzi. Hatuna mazungumzo wala makubaliano na mtu yeyote kutoka chama kingine kuhusu nafasi ya Urais. Mgombea wetu atapatikana kwa kupitia vikao vya chama chetu…’ -@zittokabwe WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment