Akizungumza na umati mkubwa uliofurika katika viwanja hivyo jana jijini Dar es Salaam, kusikiliza azima ya kiongozi huyo huku wakiwa na shauku kubwa ya kufahamu orodha ya majina hayo, Zitto alisema kuwa atawapatia karatasi waandishi wa habari yenye orodha ya majina hayo ili waende kuifanyia kazi kwa kuwahoji wahusika kulingana na taaluma yao.
Alisema kuwa mwisho wa hotuba yake angegawa karatasi kwa wanahabari yenye majina hayo, ambapo wananchi walionekana kuwa na shauku ya kupata karatasi hiyo yenye majina 99 ya wafanya biashara maarufu ndani na nje ya nchi, lakini Zitto akasema hakuwa tayari kuwapatia nakala hiyo wananchi, hivyo akawataka wafuatilie katika mitandao ya kijamii pamoja na kwenye vyombo vya habari kwani wao kwa kutumia taaluma yao wanao uhuru wa kuyaanika hadharani.
Aidha, aliongeza kuwa kati ya majina hayo ya watu wenye mabilioni ya fedha nchini Uswisi, kuna wengine wanamiliki kihalali lakini wengine wamejilimbikizia kinyume cha sheria.
“Nimeweka leo orodha ya majina hayo wazi ili kuiwezesha serikali kutoa taarifa ya uchunguzi kabla ya Bunge kuvunjwa wiki ijayo, majina 99 mtayapata kupitia kwa wanahabari niliowapatia nakala yenye orodha ya vigogo hao ama Watanzania walio na akaunti kwenye HSBC ya Uswisi ikiwa na akiba ya Dola 114 milioni za Marekani,” alisema Zitto.
Baada ya kuhitimisha mkutano hao, kiongozi huyo wa ACT aligawa karatasi hiyo kwa baadhi ya waandishi wa habari. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment