Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Video: Tazama alichokifanya Kanye West huko Canada Baada ya Mic Kupata Hitilafu Akiwa Jukwaani

Video: Tazama alichokifanya Kanye West huko Canada Baada ya Mic Kupata Hitilafu Akiwa Jukwaani

Hakuna kitu kinachokera kwa msanii awapo jukwaani , kama mitambo kuleta hitilafu ambazo zitasababisha ashindwe kutoa burudani nzuri , au wakati mwingine kufanya aonekane amefanya show mbaya.

Jumapili iliyopita Kanye West aliacha gumzo huko Toronto, Canada baada ya kukatisha onesho lake ghafla na kuondoka jukwani.

Baada ya kupanda jukwaani mbele ya watazamaji elfu 40 kwenye onesho la Pan Am Games, Kanye aliamua kukatiza onesho lake ghafla dakika ya 13 tu toka aanze kutumbuiza, na kuondoka jukwaani huku akiacha watu wamepigwa butwaa.

Uamuzi huo wa Kanye ulifuatia hitilafu ya kiufundi iliyojitokeza na kusababisha kipaza sauti alichokua akitumia kisifanye kazi ipasavyo.

Akiwa anaendelea kuwapa burudani mashabiki ghafla alirusha mic hiyo juu na kuondoka jukwaani hapo ‘like a boss’, na kuwaacha watu wakishangaa sababu hawakutarajia kuona kilichotokea.

Tazama alichokifanya Kanye:
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips