Hayo yamedhihirika hivisasa wakati Mwenyekiti wa chama hicho Rais Dkt Jakaya Kikwete akiingia kufungua mkutano huo ambapo imezoeleka wajumbe huimba kuwa na imani na Mwenyekiti ambaye ni Rais Dkt Jakaya Kikwete lakini leo hali imekuwa tofauti. Wajumbe walipaza sauti zao wakiimba wimbo wa kuwa na imani na Edward Lowassa.( Tuna Imani na Lowassa...!!! Tuna Imani na Lowassa!!)
Mkutano huo wenye wajumbe 324 kati ya 374 umehudhuriwa na wajumbe mbalimbali wakiwemo baadhi ya wanasiasa walio omba ridhaa ya kuteuliwa kugombea urais ndani ya chama hicho.
Kwa upande mwingine mtia nia aliyechujwa Prof. Mark Mwandosya yeye kwa upande wake amewashukuru wananchi kwa ushirikiano walio mpa na kusisitiza kuwa hatogombea tena ubunge katika uchaguzi mkuu ujao. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment