Akizungumza katika mkutano huo Kingunge amesema Kamati ya Maadili huko nyuma ilikuwa ni chombo cha kuandaa taarifa ili kuisadia Kamati Kuu katika kuwajadili wagombea lakini safari hii Kamati ya Maadili imefanya kazi isiyowahusu kikatiba ikiwemo kukata majina ya wagombea.
Amesema Kamati ya Maadili ya Chama cha Mapinduzi (CCM) yenyewe imekosa maadili ya kuheshimu katiba na taratibu za chama kwa kujipa madaraka ya kupeleka majina 5 kwenye kamati kuu, ambayo ilipaswa kuhoji wagombea wote 38.
“Kuna baadhi ya watu waliamua kuitumia Kamati ya Maadili kuandaa watu wao na kuwakata wengine kwa sababu zao.” Amesema Kingunge.
Kingunge amedai kwamba CCM ni chama cha wanachama wote, taratibu na kanuni zikipuuzwa na kufanya vitu kwa maamuzi ya kikundi fulani, amedai kuwa kwenye vikao vya CCM Ulifanyika uhuni na dharau kwa wanachama wengine.
"Wakubwa waliopewa madaraka wanaona hakuna lolote tunaloweza kufanya."
Amesisitiza kuwa kilichofanyika Dodoma hakikuwa sawa, Kamati Kuu iliporwa kazi yake, hii ni dharau kwa wanachama na wagombea wote. Kamati Kuu ya Taifa CCM, ipo chini ya Halmshauri Kuu ya Taifa yenye madaraka ya kujadili mapendekezo yalioletwa na Kamati Kuu, na Halmshauri Kuu ina madaraka ya kukataa au kukubali mapendekezo yalioletwa na Kamati Kuu, lakini utaratibu huo haukuwepo
Kingunge amesema anawaheshimu sana Mzee Benjamin Mkapa, Mwinyi, na Karume, lakini amesikitika kuwa ndio waliotoa michango ya kutotoa haki kwenye Kamati Kuu.
"Waliogombea 1995 walikuwa 16, Kamati Kuu iliwasikiliza na kuandaa orodha ya watu 6,” alisema Kingunge.
Akizungumzia yaliyokea NEC Kingunge amesema wajumbe walihoji kwa nini Jina La Lowassa halikuwemo, mjadala ulikuwa mgumu, watu walisema lazima aingie kwenye orodha. "......Kwa mara ya kwanza muundo wa Chama ulijaribiwa baada ya wajumbe kutaka jina la Lowassa kwenye orodha ya majina 5."
Kwa upande mwingine, amewapongeza wajumbe walijitokeza kukataa maamuzi ya Kamati Kuu ikiwemo Adam Kimbisa, Mbunge wa Songea Emmanuel Nchimbi na Sophia Simba.
Akizungumzia kauli ya Mbunge huyo kuhusishwa na ufisadi Kingunge amesema,
"Hadithi ya Lowassa kuwa ni fisadi haina mashiko, ilianza kwa kashfa ya Richmond. Kamati teule ya Bunge iliundwa na kutoa taarifa za ovyo sana, na hatimaye kwa kulinda heshima ya serikali na chama akajiuzulu."
Kingunge ameongeza kuwa Lowassa sio wa kwanza kuwajibika kisiasa .Amesema katika awamu ya kwanza ya Mwalimu –walikuwemo viongozi wa kisiasa waliouzulu.
Amewataja waliowahi kujiuzulu kuwa ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Ali Hassani Mwinyi, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na Mkurugenzi wa Usalama Taifa wote walijiuzulu kisiasa na Mwalimu aliwashukuru kwa kuwajibika.
“Lowassa alijiuzulu kuwajibika kisiasa, lakini ikabadilishwa kuonekana ni yeye ndiye aliyefanya makosa, ndio ukaanza wimbo wa ufisadi. Serikali yenyewe ilimsafisha kupitia TAKUKURU, lakini wimbo wa ufisadi ukaendelea, wakaja na wimbo mwingine wa Gamba.
“Yote haya yalipangwa na ‘Kitengo’ kilichoandaa kashfa ya Richmond. Edward ana historia ndefu ndani ya Chama.” amesema mzee Kingunge.
Amesisitiza kuwa Uongozi wa Chama na Nchi umetumia nguvu kubwa sana kupuuza wananchi wanataka nini na kuhakikisha wanayempenda hapati kitu
Ametumia mkutano huo pia kuwaomba viongozi ndani ya CCM warudi kusoma ahadi za mwanachama, warudi pia wasome utangulizi wa katiba ya CCM na kusisitiza kuwa kilichotokea Dodoma hakikubaliki, si halali na si haki. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment