MIKAKATI YATENGENEZWA KUONESHA LOWASSA ALIANZA KAMPENI MAPEMA
SIRI NYETI ZAVUJA
Wakati Chama Cha Mapinduzi(CCM) kikiendelea na hekaheka za vikao vya uteuzi wa wagombea ili kumpata mgombea atakaye peperusha chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, jaribio jipya lakutaka kumzuia kada wa chama hicho ndugu Edward Lowassa imefahamika.
Habari kutoka vikao vya ndani vya siri vilivyo kaa kuanzia juzi, jana, na leo vimeripoti kuwa mkakati huo mahususi na wa siri uliowakutanisha vigogo wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) umeazimia kumshinikiza msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mutungi kuandaa taarifa itakayo mtia hatiani ndugu Edward Lowassa kwa kuonesha kuwa alianza kampeni kabla ya wakati.
Mkakati huo wenye Baraka za vigogo wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) umeratibiwa kwa umakini mkubwa kwa msukumo wa wagombea wanatajwa kwa majina ya Bernard Membe, Mizengo Pinda, Januari Makamba na John Pombe Magufuli, ambao pia wamepata Baraka kutoka kwa baadhi ya vigogo wa Chama Cha Mapinduzi.
Mkakati huo wa kumtumia Jaji Francis Mutungi unakwenda sambamba na matamko ya hivi karibuni yaliyo ratibiwa na Mchungaji Christopher Mtikila kwa kuwataja makada wa Chama Cha Mapinduzi kuwa wamekiuka kanuni na kuvunja sheria ya uchaguzi lakini mhusika mkuu akiwa ni ndugu Edward Lowassa.
Katika mkakati huu Jaji Francis Mutungi ameshinikizwa kueleza kisheria kuwa Edward lowassa amevunja kanuni wakati wa kukusanya wadhamini pia mtoa taarifa wetu alieleza kuwa Jaji Francis Mutungi ameahidiwa nafasi nyeti serikalini endapo atafanikiwa kujenga hoja zenye mashiko ya kumtia Edward Lowassa hatiani. Alipotafutwa kwa simu, Jaji Francis Mutungi simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno pia hakujibu.
Ripoti ya mkakati huu inatarajiwa kuwasilishwa kesho mapema na Jaji Francis Mutungi kwa vigogo wa Chama Cha Mapinduzi na baadae Kamati Kuu lakini kwa masharti kwamba Jaji Francis Mutungi awahakikishie kwa hoja za kisheria vigogo hao namna ya kumtia hatiani Edward Lowassa ili apoteze sifa za kuteuliwa na hatimaye kuwa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi.
Wakati hayo yakiendelea, imeelezwa kuwa Mwenyekiti wa chama amekuwa akipata shinikizo kubwa kutoka kwa watu wasio kitakia mema Chama Cha Mapinduzi na hata shinikizo kutoka kwa familia yake kuwa Edward Lowassa akiteuliwa kuwa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi na hatimaye kushinda kiti cha urais kwamba anampango wa kulipa kisasi kwa vigogo wa serikali ya sasa.
Mwandishi wetu alipo fanya mahojiano na wajumbe wa Nec wa mikoa ya Morogoro na Mwanza juu ya mikakati hii haramu dhidi ya mdugu Edward lowassa mmoja wa waNec hao alisema “ndugu yangu sikia nikuambie unajua ni kwa nini Nape alitoa tamko kuwa muda wa kukata rufaa hautoshi, na kwa nini vikao vya maadili na kamati kuu vimesogezwa mbele hii yote ni kuanda mikakati ya kumtosa Edward Lowassa lakini nikuhakikishie ndugu yangu mwisho wa hiki chama utakuwa kesho kwenye vikao vya Nec kwa sababu mambo yote wanayo yafanya tunapata taarifa, ndugu mwandishi kama hauamini subiri kesho kwenye vikao vya Nec” alisikika mmoja wa wajumbe wa Nec kutoka mkoa wa Morogoro.
Mnyetishaji wetu huyo alitaja majina ya vigogo wanao pigiwa chepuo kuwa ni Bernard Membe, John Magufuli, Garib Bilal, January Makamba na Dr. Asha Rose Migiro huku mikakati ikiwa kumfanya Bernard Membe awe Mgombea wa CCM kwa kumwekea wagombea dhaifu.
Wakati huohuo Ndugu Sendeka aliitwa na mh Benard Membe nakutaka kumpatia kitita cha shilingi za kitanzania milioni kumi ili amsemee vizuri katika vikao vya Nec na ndugu Sendeka kukataa mradi huo.
Ni Mimi Mwalimu Julius/Jamii Forums WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment