Kwa mujibu wa mtandao wa “Africa Review ” wa Afrika kusini, umetoa orodha ya maraisi 10 wa Afrika ambao wanaingiza pesa ndefu zaidi, Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.Jakaya Mrisho Kikwete ameshika namba 4, utafiti huo umeonesha kuwa ni serikali chache zinazoweka wazi kiasi cha pesa zinazowalipa viongozi wa nchi zao, na orodha hiyo imetengenezwa kwa kuzingatia kiasi cha pesa ambacho nchi inaingiza.
Hii ndio orodha kamili
Paul Biya – Cameroon dola 601,000
King Mohammed VI – Morocco dola 480,000
Jacob Zuma – South Africa dola 272,000
Jakaya Kikwete – Tanzania dola 192,000
Abdel Aziz Bouteflika – Algeria dola 168,000
Teodoro Nguema – Equatorial Guinea dola 150,000 (makadirio)
Uhuru Kenyatta – Kenya dola 132,000
Hassan Sheikh Mohamoud – Somalia dola 120,000
Ikililou Dhoinine – Comoros dola 115,000
Denis Sassou Nguesso – Congo Republic dola 110,000
Raisi wa Cameroon Paul Biya, ameshika namba moja kwa kiasi cha dola 601,000 ambacho amemzidi raisi wa Afrika kusini ,Jacob Zuma mbali ya kuwa uchumi wa Afrika kusini umeuzidi mara 10 zaidi uchumi wa Camerron.
Kwa ujumla, utafiti unaonesha kwamba viongozi wa nchi masikini huwa wanalipwa pesa ndefu zaidi kuliko wale wa nchi zenye uchumi wa juu. Lakini kuna baadhi ya marais wanaaminika kuwa na utajiri mkubwa binafsi japo hawapo kwenye orodha hii. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment