Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Hatimaye kaka Yake Zari Amchumbia Mwanamuziki Linah Sanga....

Hatimaye kaka Yake Zari Amchumbia Mwanamuziki Linah Sanga....

Hatimaye staa wa Bongo Fleva ambaye ni zao la Nyumba ya Vipaji Tanzania (THT), Esterlina Sanga ‘Linah’ amechumbiwa rasmi na yule jamaa wake, Wiliam Bugene ‘Boss Mtoto’ ambaye ni kaka kiukoo wa mpenzi wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady.’

Akizungumza na Amani kwenye mahojiano maalum alipotimba katika Tamasha la Filamu la Kimataifa (ZIFF), Zanzibar hivi karibuni, Linah alisema kuwa ana furaha maishani mwake kwa kumpata mtu mwenye mapenzi ya kweli ambaye atafunga naye ndoa ‘soon’.

Tayari ameshanichumbia, anajulikana kwetu na mimi najulikana kwao. Kifuatacho ni ndoa yangu,” alisema Linah ambaye hivi karibuni amesema ataachia wimbo mpya utakaokuwa gumzo.

Furaha ya Linah inakuja kufuatia kumpata mwanaume huyo ambaye amekuwa akionekana naye kila kiwanja wakiwa wamegandana kimahaba ikiwa ni miezi kadhaa tangu alipodai kuporwa bwana’ke, Nagari Kombo anayedaiwa kakwapuliwa na Wema Sepetu.

Kabla ya Boss Mtoto na Kombo, huko nyuma Linah aliwahi kuripotiwa kuwa kwenye uchumba ‘serious’ na msanii mwenzake, Amini Mwinyimkuu. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips