Gwiji wa zamani wa soka la kimataifa wa Ivory Coast na klabu ya Chelsea, Didier Drogba, ni mmoja wa washambuliaji bora zaidi waliowahi kutamba katika barani Afrika, Asia na Ulaya.
Drogba ambaye alitangaza kustaafu kuichezea Ivory Coast mwaka jana, pamoja kufahamika kuwa mwiba mkali kwa mabeki wa timu pinzani wakati akiwa kwenye ubora wake, Drogba pia nae alikuwa na mabeki ambao walikuwa ni visiki zaidi kila alipokuwa anakutana nao.
Didier Drogba amemtaja nahodha wa zamani wa Barcelona na timu ya taifa ya Spain, Carles Puyol, Rio Ferdinand, na Nemanja Vidic kuwa ndio mabeki visiki zaidi aliowahi kukutana nao.
“Siku zote nimekuwa nikisema wewe Rio na Vidic ni walinzi ambao nilikuwa napata sana taabu timu zetu zinapokutana… Nilipokuwa nikifunga dhidi ya Manchester United nilikuwa nafurahia sana kwa sababu si mara nyingi nilikuwa nikipata nafasi ya kufunga dhidi yao.”
“Nyie wawili na Carles Puyol ndio mabeki ambao mlinisumbua sana, Carles alikuwa mzuri sana uwanjani na hata nje“>>> Didier Drogba.
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment