Akizungumza na Planet Bongo ya East Afrika Radio, Afande alisema Sugu ameshindwa kuwatumikia wasanii na kujinufaisha yeye mwenyewe.
“Sisi tuliamini akienda kule ndio mdomo wetu, kasahau kabisa wasanii wenzake,” alisema. “Kipindi ambacho wasanii wa antivirus wanalalamika kwamba kawatosa porini, akasema yeye sio mbunge wa wasanii ni mbunge wa Mbeya. Huyu ni msaliti kwa wenzake, sasa mtu msaliti namna hii jinsi kumuondoa ni sisi kuamua kuingia bungeni wenyewe kupigania maslahi yetu,” aliongeza.
Baada ya kauli hiyo, Sugu amemjibu kwa kusema kuwa yeye hakuwa mbunge wa wasanii bali alikuwa mbunge kwaajili ya watu wake wa Mbeya mjini.
“Nafikiri hafuatilii bunge, unajua uzuri wa vitu vya bunge vinaenda kwa rekodi, labda atakuwa hafuatili bunge. Lakini kwa wanaofuatilia bunge wanajua. Mimi sio mbunge wa wasanii, mimi ni mbunge wa Mbeya mjini,” alisema Sugu.
“Kwahiyo chochote ninachokifanya bungeni ninakifanya kwa mapenzi yangu na pia kama waziri kivuli. Kwa msanii anayefanya kazi sawa ila kwa mtu anayelala lala kama yeye lazima atakufa njaa. Lazima utakufa njaa lakini kwa msanii kama Professor Jay, msanii kama Shetta wana- appreciate kazi ambayo tunaifanya bungeni kwa kauli zao.” WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment