Kuelekea fainali ya Ligi ya Mabingwa kati ya Barcelona dhidi ya Juventus, kiungo Xavi
mwenye umri wa miaka 35 alipewa heshima katika klabu ambayo aliitumikia
kwa muda mrefu tangu ana umri wa miaka 11 alipojiunga nayo.
Fainali hiyo inayosubiriwa na watu wengi itafanyika siku ya Jumamosi.
Xavi
ameshindwa kuzuia hisia zake na kumwaga machozi wakati wa shamrashamra
za kumuaga ndani ya klabu yake ya Barcelona kuelekea fainali ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya dhidi ya Juventus.
Xavi amemshukuru kocha Luis Enrique
kwa kumuwezesha kubaki katika klabu hiyo msimu uliopita huku akishindwa
kuvumilia maneno ya Iniesta aliposimama na kumuaga kwa niaba ya
wachezaji wenzake.
Kiungo
huyo alitangaza mwezi uliopita kwamba anakwenda kumalizia soka yake
katika klabu ya Al-Sadd ya Qatar mwishoni mwa msimu, akihitimisha miaka
yake 24 kuwa na vigogo hao.
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment