Saudi Arabia inasema kuwa imezuia makombora yaliyofyatuliwa kutoka nchini Yemen kwenda ardhi yake na waasi wa Houthi.
Utawala unasema kuwa makombora hayo yalikuwa yamelenga mji wa Khamees Mushait mapema leo lakini yakadunguliwa .Shirika moja la habari lilisema kuwa raia wanne wa Saudi Arabia waliuawa na watu wengine kadha nchini Yemen wakati jeshi lilipopambana na waasi wa Houthi watiifu kwa rais wa zamani ya Yemen Ali Abdullah Saleh.
Wakazi wa mji mkuu Sanaa wanasema kuwa mji huo baadaye ulishambuliwa vikali na muungano unaoongozwa na Saudi Arabia.
Gallos Official Blog
Chanzo BBC
0 comments:
Post a Comment