Lupita Nyong’o ni moja ya waigizaji wa kike wakubwa duniani.. Kenya inajivunia huyu staa wao, alianza kuonekana kwenye movie ya ‘12 Years A Slave’..
baada ya hapo milango ikafunguka upande wake, tukamuona tena kwenye
movie ya Non-Stop.. Tayari ana Tuzo kubwa mikononi mwake na kazi ya
movies inaendelea kama kawaida yani.
Mwaka jana kulikua na fununu kua staa
huyo mpya wa hollywood ataigiza tena kwenye movie nyingine kubwa ya
Hollywood movie series ‘Star Wars Episode VII – The Force Awakens‘ alafu baadae ikawa kimya.. kipya kwenye headlines ni kwamba rasmi kabisa taarifa imetolewa kwamba Lupita atakuwepo kwenye ‘Star Wars Episode VII – The Force Awakens’.
Movie itaachiwa cinema December 18 2015 ambapo Lupita amecheza kama “Maz Kanta”.
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment