“Niko sawa, nilikubaliana na changamoto nilizopitia.. namshukuru Mungu kwa kila kitu.. nina amani na furaha." Sitti Mtemvu.
Kilichomfanya akaamua kuvua taji “Ilikuwa inaniathiri mimi na familia yangu… nikaamua nirudishe maana maneno yalikuwa mengi“
Sitti anasema mdogo wake aliumizwa pia na kila kilichomkuta yeye “Ilifikia hatua marafiki zake shule wanamtania, walikuwa wanamwambia wewe ni mtoto wa ‘bibi bomba“
Kwani alilazimishwa kuvua Taji? Uhusiano wake na Kamati ya Miss Tanzania ukoje? “Hapana, niliamua acha nivue taji.. mimi na wao hatuna tatizo kabisa"
Iliwahi kuandikwa kwamba ana uhusiano na Hasheem Lundenga, jibu lake je? “Hamna uhusiano wowote kati yangu na Hasheem Lundenga, mengi yaliandikwa kama ilivyoandikwa mimi na mtoto, it’s okay… yamepita”
Swali la umri je? “Nimeamua kufunga huo ukurasa kwa sababu chochote nitakachokisema kitafunua mambo yaliyopita.. nimeendelea mbele mimi sio Miss Tanzania nimeufunga huo ukurasa.. umri wangu ni kitu binafsi”
Exclusive hiyo nimeirekodi @EATV, hapa unaweza kuplay ukasikia sauti ya nterview yote mtu wangu.
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment