Riyama alibandika picha hiyo kuandika “………?” kitu ambacho kiliwafanya mashabiki kupoteana kabisa, wapo ambao wadai kuwa mwanadada huyo yupo lokesheni anatengeneza muvi na wenngine kudai kuwa hiyo sio muvi bali ni kweli staa huyo kwasasa ni mjamzito.
Kwa siku za hivi karibuni staa huyo amekuwa akitupia picha kadhaakwenye ukurasa wake akiwa na jamaa huyo (alimuita Baba Fatma kwenye moja ya posti zake) akimtambulisha kuwa ndio mwandani wake.
BongoMovies.com imejaribu kumtafuta Riyama ili atoboe ukweli juu ya jambo hili bila mafanikio.
Kama ni kweli, tunakupongeza na kukutakia kheri kwani ni jambo jema.
Mzee wa Ubuyu WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment