Habari kutoka chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa Lulu kilidai kwamba, mwanadada huyo amekuwa na mawasiliano ya karibu na Van Vicker tangu walipokutana Septemba, 2013 kwenye Jengo la Akade, Posta jijini Dar ambapo jamaa huyo alitua nchini kurekodi filamu na mastaa wa Bongo.
“Kwa taarifa yenu Lulu sasa hivi mambo yake na Van Vicker ni bambam na wanawasiliana usiku na mchana, nadhani kuna kitu kikubwa kinakuja. Yaani Lulu amemganda jamaa japokuwa sijajua kamili kama wana project gani.
“Kama mtakumbuka kipindi kile Van Vicker alikuja Bongo kucheza filamu ya Hashim Kambi (mwigizaji wa Bongo) ndiyo walifahamiana.
“Inawezekana anataka kufanya naye kazi kama Wema (Sepetu) ambaye hivi karibuni alikwenda Ghana na picha zikasambaa wakifanya yao,” alisema mtu huyo kwa sharti la kutochorwa jina gazetini.
Baada ya kumwagiwa ‘ubuyu’ huo, gazeti hilo lilizungumza na Lulu juu ya ishu hiyo ambapo alikiri kuwa ni mtu wake wa karibu na kwamba ni kweli amekuwa akiwasiliana naye.“Van Vicker ni mtu wangu, nimekuwa nikiwasiliana naye, kusalimiana na kuulizana maendeleo ya kazi zetu za sanaa,” alisema Lulu. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment