Ikumbukwe kuwa, ndege wenye manyoya yanayofanana siku zote huruka pamoja na kwa kuwa hii orodha ni ya watu wanaomuunga mkono Lowassa bila shaka tabia zake zitakuwa zikifanana na watu hao. Jionee mwenyewe:
1. Benjamin William Mkapa - huyu alisema mara kadhaa wakati akiwa rais kuwa Lowassa ni jembe. Hata pale Lowassa alipojiuzuru nafasi ya uwaziri mkuu Mkapa alisema kuwa, "Tusikubali kukosa viongozi wazuri na mahiri kwa kuziamini tuhuma za kipuuzi."
2. Balozi Job Lusinde ambae ni mwenyekiti wa baraza la wazee mkoani Dodoma, ambae katika utumishi wake hana hata doa la kashfa, ameeleza wazi mara kadhaa juu ya anayefaa kuliongoza taifa kwa wakati huu na amekuwa akimtaja mhe Lowassa.
3. Mzee Mwinyi, mara kadhaa mzee wetu mwinyi, rais aliyefungua milango ya neema kwa Watanzania amekuwa akiwasihi Watanzania kuhusu kumuunga mkono Lowassa katika safari yake ya matumaini. Ushahidi upo sehemu nyingi ikiwemo 'Google' kwa kuzisoma kauli zake mwenyewe.
4. Mama Maria Nyerere, mama wa taifa letu Tanzania, waziwazi akiwa na waandishi wa habari nyumbani kwake alieleza kuwa, katika vijana ambao baba wa taifa alikiri kuwa ni wa chapakazi enzi za utawala wa Mwinyi walikuwa ni Lowassa huku mwingine akiwa ni Kikwete.
5. Mchungaji Gwajima, huyu ni mchungaji wa wana kondoo zaidi ya 70,000. Kauli yake inafuatwa na wana kondoo wake. Mara kadhaa amesikika akisema yupo pamoja na Lowassa na ana muombea kwa Mwenyezi ili safari ya matumaini ifike salama.
6. Mashekhe na maustadhi wengi tu (hapa sina haja ya majina) wamekuwa wakimshawishi Lowassa kuchukua fomu ya urais. Pia hivi karibuni tumeshuhudia wengine wakiahidi kumuunga mkono huko Arusha!
8. Baraza la maaskofu la kanisa la kipentekosti wamekuwa wakimjadili Lowassa mara kadhaa na hitimisho lao kuu ni kwamba Lowassa anafaa kuongoza nchi! Maaskofu hawa wamemsafisha Lowassa dhidi ya tuhumu zote zilizoelekezwa kwake ambazo hadi hivi sasa hakuna aliyethibitisha hata moja wakati mahakama zetu zote zipo wazi!
9. Afande mstaafu Tibaigana, miongoni mwa maafande waliojizolea heshima kubwa kwa uadilifu nchini ni afande Tibaigana. Kwa maeneo kadhaa, afande mstaafu Tibaigana amekuwa akimuunga mkono Lowassa!
10. Wabunge wenye heshima kama Ole Sendeka, Lembeli, Lugola wote hawa wamekuwa wakimuunga mkono mhe Lowassa.
Je, watu hawa wote wenye heshima zao katika taifa letu na wenye kutanguliza uzalendo wa taifa lao mbele huku maslahi yao binafsi wakiyaweka nyuma, watawezaje kumuunga mkono mtu mwizi na fisadi!?!
Baadhi ya hao watu walishika nyadhifa muhimu kwa taifa na hata senti haijawahi kupotea chini ya uangalizi wao.Iweje leo wamuunge mkono mwizi?!?
...Mtanzania, tafakari. Tuhuma za ufisadi kwa Lowassa ni uzushi tu. Kama ushahidi upo, mahakama zipo wazi, kwanini hadi leo yupo uraiani?... WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment