Chumba anacholala Singano na Kaka yake Hais Ramadhani
UMAARUFU ni kama utumwa! huwezi kuwa huru kama una jina kubwa, halafu maisha yako ni ya kawaida tu.
Kuna
idadi kubwa ya wachezaji maarufu wa mpira wa mguu nchini, pia wapo
wanamuziki n.k, lakini maisha wanayoishi ni tofauti na majina yao. Ni
maisha ya kiwango cha chini.
Katika soka la Bongo, huwezi kutaja wachezaji wenye majina makubwa kwasasa ukaliacha jina la Ramadhani Singano ‘Messi’.
Singano akiwa na majirani zake
Uwezo
wa kupiga chenga, pasi, kasi na staili yake ya uchezaji ya kutumia mguu
wa kushoto akitokea winga ya kulia ni vitu vinavyofanya Singano
aonekana mahiri kusakata kabumbu.
Kila
mtu kwasasa anajua kwamba Singano ana matatizo ya kimkataba na klabu
yake ya Simba na tulieleza kwa undani siku ya jana.(Rejea habari za
jana).
Katika
stori yetu ‘exclusive’ na Singano jana, tuliahidi kuendelea na sinema
ya suala lake na leo tunakuletea sehemu ya pili ya maisha yake binafsi.
Singano anaishi kwa ndugu yake eneo la Keko, Machungwa jijini Dar es salaam.
Kiukweli;
maisha anayoishi Singano yanasikitisha mno, hana nyumba, badala yake
ameomba hifadhi kwa kaka yake, Hamis Ramadhani ambaye pia anamsimamia
mambo yake (Meneja).
Hamis na Singano ni ndugu wa damu, wamezaliwa na mama mmoja baba tofauti.
Baadhi ya picha za ukutani chumbani kwa Singano
Moja
ya vipengele katika mkataba wa Singano ni kupatiwa kodi ya nyumba,
lakini katika maisha yake yote toka asaini mkataba huo Mei 1, 2013
hajawahi kupewa hata shilingi kama anavyothibitisha mwenyewe;
“Kipengele
cha kulipiwa kodi ya nyumba hakijatekelezwa, niliuandikia barua uongozi
wa Aden Rage toka mwaka jana, lakini mpaka sasa naona kimya. Nashangaa
kitu kimoja; uongozi huu wa Rais Aveva (Evans) baada ya kuingia
madarakani unasema ulipokea nyaraka zote, sasa vipi barua yangu ya kudai
stahiki zangu hawakupewa au hawajaiona?”
SWALI:
Singano, mtandao wetu umefika unapoishi hapa Keko -Machungwa na
kushuhudia maisha yako halisi, dhahiri mazingira haya hayafanani na
umaarufu wako, unaishi chumba kimoja na kaka yako wakati kuna kipengele
cha kupewa kodi ya nyumba na hukijatimizwa, una lipi la kuwaambia
Wachezaji wa Kitanzania na Watanzania wote?.
Singano:
“Mimi kidogo nipo tofauti na wengine, kwanza kabisa wanichukulie mtu wa
kawaida, wasiamini kile wanachokiona kwenye magazeti au media.
Kwa
jina langu mimi Ramadhani Singano Messi watu wanaweza kutegemea naishi
vizuri, maisha ya hali juu, hapana! siwezi kuigiza, maisha yangu ni ya
chini sana.
Naishi
kawaida sana, nikiamka asubuhi naenda kuswali, nikirudi nakaa nyumbani
tu. Chumba tunalala chumba kimoja na kaka yangu, wakati kwenye mkataba
wamesemanitalipiwa
nyumba. Nimeomba hifadhi kwa kaka yangu. Labda watu watahisi kuna watu
wananitumia, hapana!, ninadai haki zangu, tuweke sawa mambo ya kimkataba
ili niwe huru na kuendelea kuongea na klabu yeyote”.
Kwa mazingira anayoishi Singano na wengine wengi, ni wazi kwamba wachezaji kibao wanajikuta wanashuka kiwango bila sababu.
Mchezaji hawezi kuwa huru, hawezi kuwa sawa kisaikolojia , muda wote anawaza namna ya kuikabili presha ya watu.
Kila
mtu anamjua na wengine wanahitaji kumtembelea nyumbani kwasababu ni
marafiki wa kimpira, wanamheshimu sana, lakini anapoishi hapana hadhi
kabisa, hivyo anaogopa kuwakaribisha moja kwa moja. Utacheza vizuri kwa
wakati wote?
Mazingira anayoishi Singano
0 comments:
Post a Comment