Katika hotuba yake baada ya kutangazwa msindi, Blatter amesema anajivunia mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha uongozi wake, ikiwemo kuanzishwa kwa mchezo wa soka la ufukweni (Beach Soccer).
“Tumefanikiwa kuanzisha Beach Soccer na sasa mchezo huo unachezwa kote duniani”
Akizungumzia umri wake, Blatter mwenye umri wa miaka 79 amesema kuwa umri mkubwa hauwezi kumzuia mtu kutimiza majukumu yake, na hivyo kwake umri siyo tatizo.
Tanzania imewakilishwa na Rais wa TFF Jamal Malinzi ambaye tayari alikwisha tangaza msimamo wa Tanzania kuwa ina muunga mkono Sepp Blatter, kwa maana hiyo bila shaka kura yake ni miongoni mwa kura 133 alizopata Blatter.
Kwa upande wa mpinzani wake Prince Ali bin Al-Hussein amekubali matokeo na kutangaza kujitoa baada ya awamu ya kwanza ya upigaji kura
Je, uonavyo wewe, Blatter anastahili kuendelea kuongoza shirikisho hilo ?WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment