Katika mahubiri yake jana jioni tarehe 08/05/2015 siku ya Ijumaa, Askofu Mkuu wa Makanisa ya Ufufuo na Uzima alifundisha juu ya somo liitwalo "VITA VYA HALI".
Katika somo hilo Askofu Gwajima alibainisha wazi ya kuwa sio kila mabadiliko ya hali ya hewa yanayotokea duniani ni matokea ya nguvu za kiasilia za dunia yaani Nature au ni mabadiliko ya majira ya mwaka bali wapo watu pia wenye uwezo wa kubadili hali ya hewa kwa njia za kichawi na kusababisha mafuriko makubwa, vifo, uharibifu Wa mali na hasara zinazoweza kuwarudisha watu nyuma.
Katika kudhihirisha mambo hayo Askofu Gwajima alitolea mfano mtu mmoja aliyewahi kuishi duniani aitwaye Nicolas Tesla ambaye alikua na uwezo mkubwa juu ya kubadili na kutawala(control) hali ya hewa.
Baadaye nikaunganisha ujumbe wa Askofu Gwajima na nikagundua jambo hili ni kweli kabisa baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Sadick kutangaza kuwa MVUA HIZI ZINASAIDIA SANA KUWAONDOA WATU MABONDENI pasipo kuwaza kuwa watu hawa ndio walipa kodi wake na ndio wanaomlipa mshahara wake!
Kwa maneno yale sasa tunaamini ya kuwa Sio kila mvua, mafuriko, ajali za moto, ajali za magari au kiangazi ni mambo ya asili bali mengi hutengenezwa na wanadamu(wachawi) na mashetani ili kuwaangamiza wengine.
Kabla ya kumaliza Ibada hiyo jana jioni majira ya saa moja na nusu, Askofu Gwajima ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu wa Jeshi la Bwana la Ufufuo na Uzima aliyaongoza majeshi yote kwenye maombi ya kusambaratisha mvua na mafuriko yote na hali kuwa ya kawaida.
Maarifa makubwa aliyonayo Askofu Gwajima juu ya mambo ya rohoni na mwilini umefanya watu kuzijua hila za wachawi na mashetani wenye nia ya kuangamiza watu na kuwafanya masikini kwa njia ya maji..
"Mvua imekoma kuanzia sasa na haitaharibu tena, na ninaiamuru ardhi imeze maji yote yaliyojaa juu ya nchi"... alisema Askofu Gwajima katika kumalizia ibada. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment