Tukio hilo lilijiri Alhamisi Kuu maeneo Buza jijini Dar, mishale ya saa 7:00 usiku huku jamii ikiwa katika harakati za kununua hiki na kile kwa ajili ya Sikukuu ya Pasaka iliyoadhimishwa duniani kote jana huku leo ikiwa ni Jumatatu ya Pasaka
Katika fumanizi hilo, timbwili la aina yake liliibuka baada ya mwanamke huyo mwenye mwili mkubwa, kuponyoka mikononi mwa mke aliyemnasa na kutoka nduki nje akiwa mtupu bila kujali hali hiyo.
Awali, ilidaiwa kuwa mume huyo wa mtu aliyefahamika kwa jina la baba Somoe, mkazi wa Kongowe (nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam) alimchepuka mke wake (mama Somoe) na kuanzisha uhusiano na mwanamke huyo.
Chanzo kikazidi kudai kwamba mkewe huyo alianza kutilia shaka mwenendo wa mumewe kutokana na kubadili tabia, hasa za kuwa beneti na simu hivyo alianza kumfuatilia kwa karibu.
“Katika kumfuatilia, siku moja akabaini meseji. Akamuuliza mumewe kuhusu meseji hiyo naye akawayawaya bila kuwa na majibu sahihi,” kilisema chanzo hicho.
Habari zaidi zilisema kuwa kutokana na ukweli kwamba, ndani ya nyumba yao, mama Somoe ndiyo kajaliwa uwezo wa kumiliki fedha, alimpa masharti mumewe kwamba achague mawili, watengane na aondoke na begi lake la nguo au atoe ushirikiano, ‘mwizi’ huyo anaswe.
“Mume akasema cha kufia! Akakubali kutoa ushirikiano ili mchepuko wake afumaniwe,” kilidai chanzo chetu. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment