Wamesema kama SUMATRA hawatatoa majibu mapema kuanzia Aprili 29 mwaka huu hawatokata tiketi kwa wasafiri na badala yake wataendelea na mgomo huo kwa siku saba.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam jana katika kikao cha dharura cha wamiliki wa mabasi yaendayo mikoani , Katibu Mkuu wa TABOA, Enea Mrutu, alisema SUMATRA ilikurupuka kushusha nauli bila kufanya mchanganuo na kuda.
Wamiliki hao waliafikiana kuwa yeyote atakayetoa gari lake kufanya biashara kabla hawajapata muafaka kutoka SUMATRA watamchukulia hatua za kisheria.
TABOA wameitaka serikali kurudisha viwango vya nauli za mabasi ya mikoani kwenye hali yake ya kawaida iliyokuwepo miezi michache iliyopita kwasababu bei ya mafuta imerudi juu, baada ya kushuka kwa kisingizio cha bei ya mafuta kushuka WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment