Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Majambazi Tena ! Yaua Askari Polisi Wawili Kwa Kutumia Panga na Kisha Kupora Bunduki na Kutokomea Pasipo Julikana

Majambazi Tena ! Yaua Askari Polisi Wawili Kwa Kutumia Panga na Kisha Kupora Bunduki na Kutokomea Pasipo Julikana

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Polisi Mkoa wa Pwani linaendesha oparesheni kali ya aina yake ya kuwasaka majambazi waliowavamia, kuwaua askari wawili na kumjeruhi mmoja na kisha kupora bunduki aina ya SMG.

Tukio hilo limetokea tarehe 30/03/2015 majira ya saa mbili usiku huko barabara ya Kilwa Kata ya Vikindu Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani. 
  
 Katika tukio hilo majambazI wapatao 8 hadi 10 wakiwa na mapanga na silaha zingine waliwavamia ghafla askari watatu waliokuwa kazini katika eneo la kizuizi cha Polisi kilichopo kijiji cha Kipara mpakani Kata ya Vikindu Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani.

Majambazi hao waliwashambulia ghafla askari hao kisha kupora silaha aina ya SMG ikiwa na risasi 30 ndani ya magazine na kutokomea kusikojulikana.

Majina ya askari wa Wilaya ya Kipolisi ya Mbagala waliouawa ni kama ifuatavyo:
D.2865 SGT FRANCIS,
E.177 CPL MICHAEL,
Askari mwenye namba D5573 D/SGT ALLY amejeruhiwa kwa risasi kwenye paja la mguu wa kushoto na amelazwa katika hospitali ya Temeke kwa matibabu.
  
Askari huyu kabla ya kujeruhiwa alipambana vikali na majambazi hayo kwa kutumia bunduki aliyokuwa nayo aina ya SMG ambayo walishindwa kumpora hivyo wakatokomea kuelekea pori la Vikindu.

Katika oparesheni hiyo, nguvu na mbinu zote za kipolisi zitatumika ambapo vikosi vya Dar es Salaam na Pwani vilianza kufanya oparesheni hiyo mara baada ya tukio ili kuhakikisha kwamba majambazi hao wanapatikana haraka iwezekanavyo.

Pamoja na oparesheni hiyo kali inayoendelea, Jeshi la Polisi linachunguza ili kubaini kama tukio hili linaashiria vitendo vya ugaidi au ni ujambazi wa kutumia silaha.

Natoa wito kwa wananchi wa mikoa ya Pwani na Dar es Salaam kupitia (dhana ya polisi jamii) kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa hali na mali kwa kutoa taarifa sahihi.

IMETOLEWA NA:
S.H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAMWEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips