Kajala Masanja:
Tangu aingie kwenye bifu na Wema Sepetu, kuna kundi ambalo linajiita Team Wema limekuwa likimshambulia kwa kumtukana na kumshutumu kwa mambo ambayo mengine hayana ukweli.
Hata hivyo, Kajala anaonekana kuwa mstaarabu kidogo kwani licha ya kutukanwa mtandaoni, yeye amekuwa mkimya akijua kujibizana na watu hao ambao wala hawana majina ni sawa na kuzidi kujichafulia.
Elizabeth Michael ‘Lulu’:
Huyu naye ni mhanga wa matusi mtandaoni. Kuna kundi la watu ambao linaonekana kuwa na chuki dhidi yake, huenda kutokana na mafanikio aliyonayo akiwa kwenye umri mdogo.
Lakini sasa, licha ya matusi anayoyaoga mtandaoni, amekuwa mvumilivu wa kuyaacha yapite. Watu wake wa karibu wanaeleza kuwa, licha ya kutukana sana mwenyewe wala hajui kwamba anatukanwa kwani si mtu wa kufuatilia nani kasema nini kibaya juu yake
Wema Sepetu:
Kama ilivyo kwa Kajala, huyu naye anashambuliwa sana na Team Kajala. Hawa ni watu ambao wamejitenga kuhakikisha wanamkosesha amani staa huyu.
Amekuwa akitukanwa kwa mengi lakini kwa kuwa anajua ustaa ni kama jalala, huwa hajali na anachukulia poa.
Ni mara chache sana amekuwa akinyanyua mdomo wake kuwajibu wale ambao wamekuwa wakimsema vibaya sambamba na kumtukana.
Kwa uchache hao ndiyo mastaa ambao hivi karibuni wametia fora kwa
kutukana na kutukanwa mtandaoni.
Tahadhari
Mastaa ambao ni wepesi kutukana mtandaoni wajue kwamba endapo Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete atasaini ile sheria ya makosa ya mtandaoni ya mwaka 2015, watajikuta wanaenda jela hivi hivi. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment