Siku chache zimepita toka lilipotokea tukio la kigaidi katika Chuo cha Garissa
Kenya, kwenye tukio hilo wanafunzi 148 walifariki.. kingine
kilichonifikia leo April 10 toka Kenya kinahusu uchunguzi uliofanyika
kuonesha kwamba kuna dalili za uzembe ama matumizi mabaya ya madaraka
wakati wa mikakati ya kupambana na wavamizi hao.
Taarifa za kwenye vyombo vya
habari Kenya zinasema ndege ambayo ilitakiwa isafirishe maafisa wa
Polisi kwenda kwenye Chuo hicho kwa ajili ya kupambana na wavamizi hao
ilitumiwa kwa ajili ya safari binafsi ya familia moja ambapo kuna
kiongozi mmoja anahusishwa kuruhusu ndege hiyo kufanya safari hiyo
wakati ambao ilitakiwa kuwapeleka maafisa hao Garissa.
Rubani amesema ndege hiyo iliondoka
katika uwanja wa ndege na kuwaacha makomandoo wa RECCE wakisubiri irudi
kuwachukua na kuwapeleka Garissa kuwaokoa wanafunzi.
Nimekuwekea taarifa hiyo hapa iliyoripotiwa na kituo cha K24 bonyeza play kuisikiliza…
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment