Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » HABARI kubwa toka Kenya bado ni ishu ya magaidi kuvamia Chuo Kikuu GARISSA..

HABARI kubwa toka Kenya bado ni ishu ya magaidi kuvamia Chuo Kikuu GARISSA..

Garissa_2362442f 
Kutokana na shambulio la kigaidi katika chuo cha Garissa kilichopo Kenya, baadhi ya familia bado hawajui watoto wao waliko, mzazi mmoja amesema aliongea na mtoto wake hadi dakika ya mwisho akiwa mikononi mwa magaidi hao baada ya kukamatwa.
Alikuwa akininong’oneza akiniambia yuko chini ya kitanda akaniambia tuu tumuombee akakata simu, saa sita na nusu nikaona hiyo namba ikinipigia nilikuwa naongea naye akaniambia nimeshikwa sina la kufanya akaniambia ndio hawa hapa silaha zao tunaziona, sijui ni bunduki sijui ni silaha gani walikuwa nazo
Akaniambia ndio wanataka kuongea na baba lakini baba amepatikana wako busy sana wanamharasi, tukaongea nae kidogo wakamnyang’anya simu nikaongea na hao magaidi Al Shabaab …
Akiendelea kusimulia; “wakaniambia wee mzee nakupa dakika mbili apige Somalia, akaniambia wee mzee umeshindwa kupiga simu? Kama umeshindwa kupiga simu acha mwanao asali maombi yake ya mwisho mi nasikiliza tu.. akasali maombi yake yote akaniambia umesikia amemaliza kuomba what next we sikiliza, sikiliza mwenyewe hesabu mwenyewe risasi naua kabisa nikasikia three gunshot… na akaniambia nimeuwa chimbeni shimo”– aliongea mzazi wa mwanafunzi mmoja aliyeuawa.
Tukio hili limesababisha wanafunzi 147 kufariki na wengine kujeruhiwa, kwa sasa Chuo hicho cha Garissa kimefungwa kwa muda.
Pole kwa wote ambao wameathirika kutokana na tukio hili, #RIP watu wetu waliofariki.
Sikiliza taarifa hiyo hapa iliyoripotiwa na kituo cha K24 kwa kubonyeza play…


WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips