Taarifa hizo zinasema pia hii ni baada ya majadiliano ya
muda mrefu na kufikia muafaka na mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe
anayetarajiwa kuongoza wabunge hao watatu kujiunga na chama hicho katika
mkutano mkuu wa ACT tarehe 28/3
Taarifa zaidi zinasema pia kuna wabunge wachache wa CCM na
NCCR waliofikia muafaka wa kumuunga mkono Zitto kwenda ACT ingawa idadi
yao haijajulikana.
Taarifa zaidi zinasema kuna mjumbe mmoja wa Kamati Kuu CHADEMA anatarajiwa pia kuungana na kundi hili kwenda ACT.
Wabunge hao wa Chadema inadaiwa ni wale mizigo ambao hawana
ushawishi wowote ndani ya chama hicho na ambao wana uhakika hawawezi
kupitishwa tena kugombea.
Tunatarajia kuwawekea hapa majina yote kamili siku chache
zijazo baada ya uchunguzi wetu kukamilika kwani tuna vyanzo vyetu vya
habari ndani ya mazungumzo hayo ingawa ni ya siri sana.
Zitto Kabwe amekuwa akikaririwa mara kadhaa kusema hatma yake kisiasa ataitangaza mwezi huu
0 comments:
Post a Comment