Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Padri FEKI Akamatwa Baada ya Kusalisha Misa Huko Morogoro

Padri FEKI Akamatwa Baada ya Kusalisha Misa Huko Morogoro


Jeshi la Polisi mkoani Morogoro, linamshikilia mkazi wa Manispaa hiyo, Josephat Asenga (47), mwenye taaluma ya uhasibu, kwa tuhuma za kujifanya Padri.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo, alisema kuwa, Asenga alikamatwa juzi saa 10:30 jioni, katika maeneo ya Modeco, Kata ya Mazimbu katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Maria.

Kwa mujibu wa Kamanda Paulo, mtuhumiwa huyo alifika parokiani hapo Juni mwaka jana akiwa amevaa mavazi ya Padri na kujitambulisha kwa Paroko wa parokia hiyo, Malt Dyfrig Joseph, kuwa yeye ni Padri anaishi Jimbo la New York Marekani.

Kwa mujibu wa kamanda huyo, baada ya kujitambulisha kwa Paroko huyo na kuonesha kitambulisho chake, alimuomba Paroko huyo kumpangia zamu ya kuendesha Misa ya Jumapili iliyofuata na kukubaliwa na Paroko huyo bila kukagua vizuri kitambulisho chake.

Alisema mara baada ya misa hiyo, Paroko alipata taarifa kutoka kwa msamaria mmoja wa Kituo cha Amani cha Chamwino mjini hapa, kuwa Padri huyo feki anaishi na mwanamke katika maeneo ya Ujenzi kinyume na taratibu za upadri.

Baada ya kupata taarifa hizo, inadaiwa Paroko huyo aliwaomba waumini wamshawishi Padri huyo feki, afike parokiani hapo na baada ya kufika, alihojiwa na Paroko huyo na kudai kuwa alipata upadrisho katika Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa kamanda huyo, baada ya Paroko huyo kupata maelezo hayo alifanya mawasiliano na Katibu wa Jimbo hilo la Dar es Salaam na kujibiwa kuwa hakuna jina la Padri huyo.

Juzi Alhamisi majira ya saa 10:30, Padri huyo feki alimpigia simu Paroko huyo na kumuomba ampange kuendesha Misa Takatifu ya Jumapili parokiani hapo, na kukubaliwa na paroko huyo na kumtaka afike kanisani.

Baada ya kufika, taratibu za kujulisha Polisi zilifanywa na askari walipofika kanisani hapo, walimkamata mtuhumiwa huyo.

Kwa mujibu wa Kamanda huyo, baada ya kufanya mahojiano na mtuhumiwa, alikiri kuwa yeye sio Padri na   walipokwenda nyumbani kwake kwa ajili ya kufanya upekuzi, walimkuta akiwa na majoho saba ya upadri.

Mtuhumiwa huyo ameendelea kushikiliwa Polisi na atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips